Kiswahili msaada : Trosolwg
Sensa ni nini?
Sensa ni utafiti ambao hufanyika kila baada ya miaka 10 na hutupa uelewa wa watu wote majumbani Uingereza na Wales. Sensa ifuatayo itafanyika Jumapili tarehe 21 Machi Mwaka 2021.
Taarifa itakayokusanywa itasaidia kupangilia na kulipia huduma za umma katika maeneo ya wenyeji, ikiwa ni pamoja na huduma za lugha. Kwa mfano, NHS inaweza kuhitaji kutoa huduma za kutafsiri kwa maandishi au kwa masimulizi katika eneo maalumu.
The Office for National Statistics (Ofisi ya Mipango ya Takwimu za Taifa) (ONS) hupanga na kuendesha sensa Uingereza na Wales.
Nani anatakiwa kujaza sensa
Sensa huuliza maswali kuhusu wewe na makazi yako, na ni muhimu kwa kila mtu Uingereza na Wales kuhusishwa.
Kisheria ni lazima kushiriki kwenye sensa
Ni kosa kutoa taarifa za uongo au kutoshiriki katika sensa na utaweza kutozwa faini isiyozidi £1000. Maswali mengine yameonyeshwa kuwa si ya lazima. Si ukiukwaji wa sheria kutoyajibu.
Kuishi Uingereza kwa muda wa chini ya miezi mitatu
Huwajibiki kujaza sensa kama unakaa Uingereza kwa muda wa chini ya miezi mitatu. Mmiliki wa makazi yako anaweza kukuuliza maswali machache ili aweze kujaza sensa kuhusu watu wanaokaa nyumbani kwake.
Ni wakati gani wa kukamilisha kidadisi chako cha sensa
Nyumba zote zikamilishe kidadisi cha sensa tarehe 21 Machi 2021, au punde baadaye.
Inawezekana kwamba hali yako imebadilika wakati wa janga la korona. Jibu maswali yote kutokana na hali yako ilivyo sasa.